Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, ofisi ya Ayatollah Sayyid Ali Husseini Sistani leo, Alhamisi, tarehe 21 Muharram 1447 Hijria (sawa na 17 Julai 2025 Miladia), imetoa tamko rasmi huku ikitoa pole kwa watu wa mji wa Kut kufuatia tukio hilo la kutisha la moto uliotokea katika mojawapo ya vituo vya biashara vya mji huo.
Matini ya ujumbe huo ni kama ifuatavyo:
Bismillāhi r-Raḥmāni r-Raḥīm
(إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ)
Watu wapendwa wa mji wa Kut
As-salāmu ʿalaykum wa raḥmatullāhi wa barakātuh
Kwa masikitiko na huzuni kubwa tumepokea habari ya tukio hili la kuhuzunisha la moto uliotokea katika mojawapo ya vituo vya kibiashara vya mji wenu mpenzi, ambalo limepelekea vifo vya watu wengi waliokuwa wakitembelea eneo hilo na kuwajeruhi wengine wengi.
Tunatoa mkono wa pole na rambirambi kutokana na msiba huu mkubwa, hasa kwa wafiwa na ndugu wa marehemu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awajalie mashahidi hawa wema rehema na msamaha wake mpana, azipe familia zao subira na uvumilivu, na awaponye majeruhi wote kwa haraka.
وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّهِ الْعَلِيِّ الْعَظِيمِ
Ofisi ya Ayatollah Sistani – Najaf Ashraf
Inafaa kuashiria kwamba Muhammad Jamil al-Mayahiy, gavana wa mkoa wa W'asit, mapema leo Alhamisi alitangaza kuwa katika tukio hilo la moto lililotokea kwenye kituo kimoja cha kibiashara katika mji wa Kut, mashariki mwa Iraq, takriban watu 50 wamepoteza maisha.
Maoni yako